Wazazi wa wasichana wa Chibok waandamana

Image caption Wasichana wa Chikok walitekwa siku 600 zilizopita

Mamia ya wazazi wa wasichana wa shule ambao walitekwa nyara katika mji ulio kaskazini mashariki mwa Nigeria wa Chibok wameandana katika mji mkuu wa Abuja.

Walikuwa wamejawa na husuni wanapoadhimisha siku 600 tangu watoto wao watekwe nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.

Image caption Wana matumaini ya kumuona rais

Lengo la wazazi hao ni kukutana na rais Muhammadu Buhari, ambaye aliwashangaza alipotangaza kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha wasicha hao wako wapi.

Baadhi ya wazazi wamegadhabishwa na waliketi kati kati ya barabara huku wakilia.