Mlipuko waua watu watano Uturuki

Image caption Maafisa wamewalaumu wanamgambo wa chama cha PKK kwa mlipuko huo

Mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari umetokea katika makao ya polisi kusini mashariki mwa Uturuki ambapo watu watano waliuawa na wengine takriban 39 kujeruhiwa.

Mwanamke na mtoto ni miongoni mwa wale waliouawa. Waokoaji wanaendelea kutafuta kwenye vifusi katika wilaya ya Cinar iliyo mkoa wa Diyarbarik.

Maafisa wamewalaumu wanamgambo wa chama cha PKK kwa mlipuko huo. Hakuna kundi lililotangaza kuhusika kwenye shambulizi hilo.

Bomu hilo lililipuliwa kwenye lango la jengo la polisi katika wilaya ya Cinar. Mlipuko huo pia uliharibu majengo yaliyokuwa karibu ambapo mama na mtoto wake waliuawa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maafisa wamewalaumu wanamgambo wa chama cha PKK kwa mlipuko huo

Inaripotiwa kuwa washambuliaji pia walifyatua makombora kwenda kwa majego hayo ya polisi.

Kulingana na vyombo vya habarin kituo kingine cha polisi kilicho katika mji wa Midyat katika mkoa ulio karibu wa Mardin pia kilishambuliwa na wanamgambo.

Mkoa wa Diyarbakir umeshuhdiwa ghasia kati ya wanamgambo wa PKK wa wanajeshi wa Uturuki miezi ya hivi ya majuzi.