Marekani yaweka sheria za kulinda simba

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Marekani yaweka sheria za kulinda simba

Simba walioko barani Afrika watalindwa zaidi mwaka huu kufuatia kuuawa kwa simba maarufu aliyejulikana kama Cecil nchini Zimbabwe na Daktari kutoka Marekani mwaka wa 2015.

Marekani imeweka sheria kali zaidi kudhibiti uagizaji wa vito vilivyotengenezwa na mabaki ya simba waliouwa.

Sheria hiyo itaanza kutetekelezwa tarehe 22 mwezi huu, na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuagiza vito vilivyotengenezwa kutoka kwa wanyama pori.

Aidha taasisi inayosimamia na kuthibiti uuzaji wa vito vilivyotengenezwa na mabaki ya wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia, pia inatarajiwa kuimarisha hadhi ya Simba duniani.

Haki miliki ya picha
Image caption Daktari Walter Palmer raia wa Marekani alimuua Simba Cecil katika mbuga ya wanyama ya Hungwe nchini Zimbabwe Julai mwaka uliopita.

Idadi ya Simba barani Afrika imepungua kwa asilimia hamsini tangu miaka ya tisini.

Jamii ya kimataifa iliangazia zaidi hatma ya Simba barani Afrika, baada ya Daktari mmoja Walter Palmer raia wa Marekani kumuua Simba Cecil katika mbuga ya wanyama ya Hungwe nchini Zimbabwe Julai mwaka uliopita.

Disemba mwaka wa uliopita shirika la wanyama pori nchini Marekani, lilitangaza kuwa simba wote kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika watawekwa katika kitengo maalum cha wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

Tangazo hilo litakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa itakuwa vigumu kwa watalii na wawindaji kuagiza vichwa vya simba, kucha na ngozi kutoka maeneo hayo.