Vladimir Putin afana kwenye mtihani Uganda

Putin
Image caption Jina la mwanafunzi huyo kwenye gazeti moja la Uganda

Mwanafunzi aliyepewa jina la Rais wa Urusi Vladimir Putin ni miongoni mwa wanafunzi waliofanya vyema zaidi mtihani wa kitaifa nchini Uganda.

Vladimir Putin alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa wa kumaliza shule ya msingi.

Mwanafunzi huyo alifanyia mtihani shule ya Kampala Quality PS.

Image caption Putin ameongoza Urusi kama Rais tangu Mei 2012

Mwandishi wa BBC mjini Kampala Patience Atuhaire anasema ni kawaida kwa wazazi nchini Uganda kuwapa watoto wao majina ya watu maarufu.

Putin ameongoza Urusi kama Rais tangu Mei 2012.

Aliongoza kama rais awali kuanzia 2000 hadi 2008, na kama Waziri Mkuu wa Urusi 1999 hadi 2000 na tena 2008 hadi 2012