Walioongoza 'mapinduzi' Burundi wafungwa maisha

Image caption Cyrille Ndayirukiye

Mahakama moja nchini Burundi imewahukumu majenerali wa jeshi walioongoza mapinduzi dhidi ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kifungo cha maisha.

Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine tisa miaka 30 jela kwa jukumu lao katika jaribio hilo la mapinduzi .

Wanne hao watakaohudumia kifungo cha maisha jela ni aliyekuwa waziri wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye,Jenerali Zenon Ndabaneze, Juvenal Niyungeko na Hermenegilde Nimenya aliyekuwa kamishana wa polisi.

Upande wa mashtaka uliiagiza mahakama kuwafunga washtakiwa wote kifungo cha maisha baada ya kukiri kushiriki katika jaribio hilo la mapinduzi mnamo mwezi Mei. .