Hiddink:'Tishio la Chelsea kushushwa lipo'

Haki miliki ya picha PA
Image caption Guus Hidink

Uwezekano wa kilabu ya Chelsea kushushwa hadi daraja la kwanza la ligi kuu ya Uingereza upo,kaimu mkufunzi wa kilabu hiyo Guus Hidink amesema.

The Blues wako katika nafasi a 14,ikiwa pointi sita juu ya timu tatu zinazokabiliwa na tishio la kushushwa katika ligi hiyo,na inatarajiwa kuchuana na Everton na Arsenal katika mechi zinazofuatia.

''Ni Kweli'',alisema Hiddink,ambaye alichukua timu hiyo kutoka kwa kocha Jose Mourinho mnamo mwezi Disemba.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho

''Tuna mechi mbili ngumu zinazofuata.Iwapo hutapata pointi za kutosha,hujui wengine watafanya nini.Ligi ya Uingereza inaweza kukushangaza''.

Chelsea ilikuwa pointi moja juu ya timu tatu zinazokabiliwa na tishio la kushushwa dara wakati Mourinho alipoondoka.