Netflix kuwazuia 'wezi' wa huduma yake

Haki miliki ya picha
Image caption Netflix

Kampuni inayotoa video za moja kwa moja mitandaoni Netflix imesema kuwa itawazuia wateja wake kutumia mtandao ili kuweza kuona kanda za video ambazo hajirahusiwa nchini mwao.

Kutokana na makubaliano ya leseni,huduma za Netflix zinatofautiana katika kila taifa,watumiaji wengi hutumia mtandao wa kibinafsi wa VPN ama maajenti wengine kuona kanda hizo.

Netflix ilipanua huduma zake kwa zaidi ya mataifa 130 wiki iliopita.

Lakini mataifa mengine yana huduma zaidi ya mengine ,kwa mfano Netflix nchini Australia ina asilimia 10 ya huduma hiyo kwa wateja wake.

David,Fullagar,naibu wa rais wa usambazaji wa huduma hiyo amesema katika blogi yake kwamba kampuni hiyo ya Marekani iko katika harakati ya kuhakikisha kuwa inatoa leseni kwa wale wote wanaotumia huduma hiyo duniani.

Hatahivyo amesema kuwa itachukua mda mrefu kwa wateja kuweza kuona filamu na vipindi sawa kila mahali.

''Iwapo huduma yetu ingekuwa inapatikana duniani,kusingekuwa na sababu ya watu kutumia maajenti wengine ili kudanganya kwamba wako katika mataifa mengine ilhali ni uongo'',alisema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Netflix

''Kwa sasa tutaendelea kuheshimu na kutoa lesini kwa wateja wetu kupitia maeneo ya kijiografia.Wateja wanaotumia maajenti wengine ili kujipatia huduma zetu nje ya mataifa yao wataruhusiwa kupata huduma hizo wakiwa ndani ya mataifa yao pekee katika kipindi cha juma moja lijalo'',ilisema kampuni hiyo.

''Wale wasiotumia maajenti ama njia nyengine hawataathiriwa na msako huo'',aliongezea.

Hatua hiyo ni kinyume na ripoti za kamouni hiyo wiki iliopita kwamba itawazuia maajenti kupata huduma yake.