Buhari aagiza kuchunguzwa kwa wanajeshi 17

Haki miliki ya picha
Image caption Sambo Dasuki

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kuchunguzwa kwa maafisa 17 wa kijeshi wanaohusishwa na ufisadi.

Tume ya uchumi na uhalifu wa maswala ya kifedha itaangazia ununuzi wa vifaa vya kijeshi kutoka mwaka 2007 hadi 2015.

Mmoja wa wale watakaochunguzwa ni aliyekuwa mshauri wa mambo ya usalama Sambo Dasuki ambaye hapo awali alakimatwa kwa madai ya wizi wa dola bilioni 2.

Image caption Muhammadu Buhari

Alishtumu utowaji wa kandarasi bandia kununua ndege 12 aina ya helikopta ,ndege nne za kijeshi na risasi.

Amekana madai hayo.