Trump na Cruz walumbana katika mjadala

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump na Cruz

Anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa sasa katika chati ya kugombea urais wa Marekani katika chama cha Republican Donald Trump na mgombea mpinzani wake Ted Cruz wameanza mjadala wao kupitia televisheni ikiwa ni malumbano makali baina yao .

Huku Trump akiushuku uhalali wa Ted Cruz kuwania urais Marekani kwani alizaliwa Canada.

Ted Cruz kwa upande wake amemwambia analeta swala hilo kwa sababu tu Trump anaelekea kushindwa katika uchaguzi wa chama hicho unaofanyika katika jimbo la Iowa wiki mbili zijazo.

Wagombea 7 wanashiriki katika mdahalo huo ambao ni katika raundi ya mwisho kabla kura za awali za chama hicho kuanza kupigwa kumchagua rasmi atakayepeperusha bendera ya Republicans katika kinyanganyiro hicho.