Afisa wa serikali aiba barabara Urusi

Vipande vya barabara
Image caption Vipande vya barabara

Wachunguzi wa Urusi wamemshtumu kaimu naibu wa huduma za magereza nchini humo kwa kuiba barabara kuu.

Afisa huyo Protopopov anadaiwa kupanga na kuharibiwa kwa barabara ya kilomita 50 iliopo eneo la mashambani kaskazini mwa Urusi na baadaye kuuza vipande vya saruji ya barabara hiyo ili kujipatia faidi.

Afisa mwengine wa magareza pia naye anatuhumiwa kutekeleza kitendo hicho cha uhalifu.

Barabara hiyo iliojengwa na vipande hivyo vipatavyo 7000 iliharibiwa na kufutiliwa mbali kwa zaidi ya mwaka mmoja katika 2014 na 2015.

Haki miliki ya picha .
Image caption Barabara kuu

Vipande hivyo baadaye vilichukuliwa na kampuni moja ambayo iliviuza na kujipatia faida,kuliingana na uchunguzi.

Protopopov, kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya utumiaji m'baya wa mali ya serikali kwa kutumia wadhfa wake ambayo huenda yakasababisha afungwe kwa kipindi cha miaka 10 jela.