Ndege za kijeshi za Marekani zagongana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za kijeshi za Marekani

Ndege mbili za wanajeshi wa Marekani aina ya helikopta zimegongana karibu na kisiwa cha Hawaii cha Oahu zote zikiwa na abiria sita.

Mkuu wa walinzi wa pwani hiyo Sara Mooers amesema kuwa mabaki yalipatikana baharini,lakini bado haijabainika ni vipi ajali hiyo ilitokea.

Kapteni wa jeshi hilo Timothy Irish ameliambia shirika la habari la AP kwamba usakaji na uokoaji ulikuwa unaendelea.

Ndege hizo zinatoka katika kitengo cha kwanza cha jeshi hilo lililo na kambi yake huko Hawaii.