Meya awatuma wahamiaji kwa Merkel

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Basi la wahamajia waliotumwa kwa Angela Merkel

Meya wa mji mmoja jimbo la Bavaria ambaye anapinga sera ya Ujerumani kuhusu wahamiaji ametuma basi moja lililojaa wahamiaji wa Syria kwa afisi ya Chansela Angela Merkel mjini Berlin.

Hata hivyo amelazimika kuwalipia mahala pa kuishi.

Peter Dreier, ambaye ni meya wa mji wa Landshut, amesema kwamba alitaka kutoa ishara kwamba sera za wahamiaji za Ujerumani haziwezi kufanya kazi kama ilivyokuwa awali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wakiwa ndani ya basi

Basi hilo liliwasili mjini Berlin siku ya Alhamisi jioni.

Wale wote waliokuwa ndani yake walijitolea kufanya safari hiyo kulingana na baraza la mji huo.

Ujerumani iliwachukua wahamiaji milioni 1.1 mnamo mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Angela Merkel

Bwana Dreier alisema kuwa alimweleza bi Merkel kuhusu basi hilo kupitia njia ya simu mnamo mwezi Octoba.