Dawa ya maafa:Kampuni yasema ilifuata utaratibu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dawa ya majaribio

Kampuni ya utengenezaji wa madawa yaliyosababisha mtu mmoja kufa ubongo katika majaribio yake katika dawa imesisitiza kuwa ilifuata utaratibu unaofaa katika kufanya majaribio hayo.

Serikali ya Ufaransa imesema kuwa watu wengine watatu wataharibika ubongo kabisa kutokana na jaribio hilo la dawa iliyokuwa inatengenezwa na kampuni moja ya Ureno ijulikanayo kama Bial.

Watu wengine wawili wako hospitalini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bio Trial

Baada ya kuwatembelea wagonjwa hao katika hospitali, Waziri wa Afya wa Ufaransa, Marisol Touraine alitaja hali hiyo kama ambayo haikutarajiwa.

Kampuni ya Bial imesema itashirikiana na wachunguzi kugundua ni kitu gani kilienda mrama.