Msemaji wa upinzani ashtakiwa na Ufisadi,Nigeria

Image caption Ufisadi nchini Nigeria

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria ameshtakiwa kwa ulanguzi wa pesa katika kashfa inayozidi kukua kuhusiana na matumizi mabaya ya pesa zilizokusudiwa kupambana na wapiganaji wa kundi la itikadi kali la Boko Haram.

Image caption Sambo Dasuki

Msemaji wa People's Democratic Party, Olisah Metuh, amekanusha kuwa alipokea dola milioni mbili kutoka kwa afisi ya Mshauri wa maswala ya usalama wa Nigeria, wakati wa enzi za Rais Goodluck Jonathan.

Image caption Mahakama nchini Nigeria

Inadaiwa pesa hizo zilitumiwa wakati wa kampeni za kisiasa na mahitaji ya kibinafsi.

Awali mshauri wa zamani wa maswala ya usalama nchini humo, Sambo Dasuki, alikanusha mashtaka ya ufisadi.