Mateka watakiwa kuachwa huru Burkina Faso

Haki miliki ya picha Djibo soutient Dr. Ken Elliot
Image caption Dr.Ken akiwa na mkewe Jocelyn

Watu nchini Burkina Faso wanafanya kampeni kushinikiza kuachiwa huru kwa daktari Raia wa Australia na mkewe, waliotekwa nyara siku lilipotokea shambulio mjini Ouagadougou.

Ken na Jocelyn Elliot, 80, wamejenga vituo vya afya tangu miaka ya 70 mjini Djibo karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na Mali.

Wakazi wameanza kampeni hizo katika mtandao wa Facebook wakituma ujumbe wenye kukemea kutekwa kwao.

Haijulikani ikiwa kutekwa kwao kunahusishwa na shambulio la ijumaa la Al Qaeda mjini Ouagadougou.

Serikali ya Burkina Faso imesema watu 28 waliuawa na wengine takriban 56 walijeruhiwa kwenye shambulio la siku hiyo lililolenga Hoteli mbilli na mgahawa ambao hutembelewa mara nyingi na raia wa kigeni.Miongoni mwa waliopoteza maisha watu sita ni raia wa Canada.