Nduguye Celine Dion afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Celine Dion

Nduguye mkubwa wa nyota wa muziki wa bluz Celine Dion amefariki kutokana na saratani ,siku mbili tu baada ya mumewe mwanamuziki huyo kufariki.

Daniel Dion mwenye umri wa miaka 59 alifariki siku ya jumamosi karibu na mji wa Montreal kulingana na taarifa iliotolewa na msemaji wa mwanamuziki huyo.

Familia ya Bi Dion ilitoa heshima zoa kwa baba huyo wa watoto wawili ikisema alikuwa mungwana na mtu mwenye vipaji vingi.

Mumewe na aliyekuwa meneja wake Rene Angelil,alifariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 73.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Celine Dion na marehemu mumewe

Kifo chake mjini Las Vegas kilijiri baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya umiyo.

Daniel Dion alikuwa mwana wa nane kati 14 na alicheza muziki na wanawe katika piano ya wazazi wake mkoani Quebec.