Israel yachukizwa na kuondolewa kwa vikwazo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema Iran ingali na azma ya kuunda zana za Nuklia na mjini Washington spika wa Paul Ryan wa chama cha Republican, amesema Taifa la Iran ambalo linaongoza kwa ufadhili wa ugaidi, huenda ikatumia fursa hiyo kuwafadhili vitendo vya kigaidi duniani.

Hatahivyo sio mataifa yote yaliochukizwa na mkataba huo .

Haki miliki ya picha AP
Image caption John Kerry na Javad Zarrif

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ameitaja hatua ya kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Iran kuwa ya kihistoria, akisema kuwa pande zote zimetekeleza wajibu wao.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza na Ujerumani nao wameitaja kuwa ushindi mkubwa wa juhudi za kidiplomasia.