Iran yawaachilia wafungwa wa Marekani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption John Kerry

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry Amesema kuwa amepata habari kuwa raia watano wa Marekani, wameachiliwa huru nchini Iran.

Amesema wafungwa hao wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani hivi karibuni.

Wanne kati yao, wana uraia wa Marekani na Iran kwa pamoja.

Mwengine ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Washington Post, ambaye alifungwa jela kwa madai ya ujasusi mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha MEHR
Image caption Wafungwa nchini Iran

Wafungwa hao wameachiliwa kama sehemu ya kubadilishana wafungwa kati ya Marekani na Iran.

Marekani kwa upande wake imewaachilia huru wafungwa saba waliokuwa gerezani nchini humo.

Kerry amesema licha ya mpango huo wa kubadilishana wafungwa hakuhusiani moja kwa moja na mazungumzo ya Nuklia na Iran, kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia na Tehran kutasaidia kuwaachilia wafungwa zaidi.