TCRA yavifunga vituo vya habari TZ

Image caption TCRA

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA imevifungia vituo vya Radio na Television kwa muda wa miezi 3 kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM.

Vituo hivyo vimefungiwa kutoa huduma kwa miezi mitatu kila moja baada ya kushindwa kulipa kodi

Kulingana na mtandao wa jamii Forum,mnamo mwezi July 2015 Serikali ilitoa taarifa kwa umma na TCRA kwamba baadhi ya radio na Televisheni zipatazo 40 zinadaiwa ada na tozo mbalimbali.

Aidha Serikali iliviagiza vituo hivyo kuhakikisha kuwa vimelipa ada kufikia tarehe 31 mwezi Disemba 2015.

Hatahivyo baadhi ya vituo hivyo vililipa kodi hiyo mwanzoni mwa mwezi huu na wengine wakishindwa kulipa.

Kwa mujibu wa sheria unaposhindwa kulipa kodi TCRA huchukulia kwamba haupo.

TCRA sasa inasema kuwa iwapo miezi mitatu ijayo itakamilika bila malipo hayo kufanywa basi italazimika kuchukua hatua zaidi kama vile kuwapokonya leseni wahusika.

Ni vituo 11pekee kati ya vituo vilivyokuwa vikidaiwa na mamlaka hiyo vilivyotiii agizo hilo na kulipa.

Baadhi ya vituo hivyo ambavyo havitakuwa hewani kufikia jumatatu ni

1. Sibuka FM 2. Breez FM 3. Country FM 4. Ebony FM 5. Hot FM 6. Impact FM 7. Iringa Municipal TV 8. Kiss FM 9. Kitulo FM 10. Kifimbo FM 11. Mbeya City Municipal TV 12. Radio 5 13. Radio Free Afrika (RFA) 14. Musa Television Network 15. Pride FM radio 16. Radio Huruma 17. Radio Uhuru 18. Star TV 19. Rock FM Radio 20. Standard FM radio 21. Sumbawanga Municipal TV 22. Tanga City TV 23. Top Radio FM limited 24. Ulanga FM