Mvua kubwa yaua 3 Bujumbura

Image caption Mvua kubwa yaua watatu Bujumbura

Takriban watu watatu wameuwa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kushuhudiwa mvua kubwa jana usiku katika wilaya ya Mutambua karibu na mji mkuu wa Burundi Bujumbura.

Radio ya taifa ya nchini humo ilitangaza kuwa karibu nyumba 90 ziliharibwa.

Pia barabara inayoelekea katika bwawa la kuzalisha umeme katika eneo hilo nayo iliharibiwa.

Kila kunapotekea mvua kubwa nchini Burundi mji mkuu Bujumbura na vitongoji vyake hukubwa na mafuriko ambavyo huchangia kutokea kwa maporomoko ya udongo na kisha maafa.