Gazeti la Mawio lapigwa marufuku TZ

Image caption Raia wa Tanzania wakisoma magazeti.

Serikali ya Tanzania imelipiga marufuku gazeti la mawio linalotolewa kila wiki kwa kuchochea ghasia.

Hatua hiyo inajiri siku chacha baada ya kuondolewa kwa marufuku ya gazeti la kieneo la The East African ,ambalo lilipigwa marufuku mapema mwaka uliopita.

Waziri wa habari Nape Nauye amesema kuwa habari za Mawio zinakiuka sheria ya magazeti.

Sheria hiyo kwa mda mrefu imekosolewa kama iliopitwa na wakati na kuzuia uhuru wa kujieleza.

Sheria inampa waziri wa habari uwezo wa kupiga marufuku ama hata kulisimamisha kwa mda gazeti lolote.

Baraza la vyombo vya habari nchini Tanzania MCT limesema kuwa limekasirishwa na marufuku hiyo.

''Tulidhani kwamba serikali mpya itatumia njia nyengine katika kukabiliana na vyombo vya habari vilivyokosa,lakini inaonekana kwamba hakuna lililobadilika,alisema katibu mkuu wa MCT kajubi Mkajanga.