Matajiri 1% wanawazidi watu wengine wote

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mashua za kifahari za watu matajiri mjini Monaco

Asilimia moja ya watu matajiri kwa sasa wanamiliki utajiri sawa na ule unaomilikiwa na watu wengine wote duniani, kulinaga na shirika la Oxfam.

Kutokana na takwimu kwenye ripoti moja ambao inawashauri viongozi wanakutana mjini Davos kuchukua hatua kuleta usawa, Oxfam pia imegundua kuwa watu 62 duniani wanamiliki utajiri sawa na nusu ya watu maskini duniani.

Oxfam ilifanyia makadirio utajiri wa pesa taslim na mali yenye thamani ya dola 68,800 sawa na na pauni 48,300 kuingia katika kundi la kwanzai la asilimia 10 ya matajiri na dola 760,000 au pauni 533,000 kungia katika asilimia moja ya matajiri.

Hii inamaana kuwa ikiwa unamilika nyumba mjini London bila ya mkopo unaingia katika kundi la asilimia moja ya matajiri.

Oxfam inazitaka serikali kuchukua hatua ili kupunguza pengo lililopo kati ya watu matajiri na maskini.

Pia inataka kumalizika kwa pengo kwa mishahara kwa misingi ya jinsia, kifidia wale hawajalipwa na kuwepo usawa wa urithi kati wa wanaume na wanawake.