Wikipedia yaadhimisha miaka 15

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mbaka sasa mtandao wa Wikipedia umefanyiwa uhariri mara 808,187,367.

Mtandao wa Wikipedia unaadhimisha miaka 15 tangu uanzishwe kwa kutoa orodha ya kura zilizofanyiwa uhariri zaidi.

Ukurasa wa kiingereza ambao kila mtu anaweza kufanyia uhariri, una nakala zaidi ya milioni tano na ulisahihishwa mara milioni 808.

Ukurasa kumuhusu rais wa zamami wa mareknai George Bush ulikuwa wenye mvuto mkubwa na ulisahihishwa mara 45,862 tangu uundwe.

Kurasa za Britney Spears, Adolf Hitler na orodha ya vipindi vinavyotangazwa na kituo cha runiga cha ABS-CBN pia zilichukua nafasi 15 za kwanza.

Mbaka sasa mtandao wa Wikipedia umefanyiwa uhariri mara 808,187,367.

Orodha kamili ya kurasa zilizafanyiwa uhariri zaidi katika mtandao wa Wikipedia ni hizi zifuatazo.

George W Bush (45,862 edits)

Orodha ya watu wa WWE (42,836)

Marekani (35,742)

Wikipedia (33,958)

Michael Jackson (28,152)

Kanisa Katoliki (26,421)

Orodha ya vipindi vya ABS-CBN (25,188)

Yesu (25,084)

Barack Obama (24,708)

Adolf Hitler (24,612)

Britney Spears (23,802)

Vita vya pili vya Dunia (23,739)

Vifo vya mwaka 2013 (22,529)

The Beatles (22,399)

India (22,271)