Watu watatu wauawa Burundi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu watatu wauawa Burundi

Watu watatu akiwemo afisa wa polisi, wakili na afisa ya cheo cha juu katika wizara ya elimu waliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa jana katika eneo moja lililo kati kati mwa mji mkuu wa Burundi Bujumbura.

Maiti mbili za wanaume waliotoweka kusini mwa mji wa Bujumbura wiki iliyopita nazo pia zilipatikana leo asubuhi.

Ghasia za kisiasa zimekuwa zikishuhudiwa nchini Burundi tangu mwezi Aprili wakati rais Pierre Nkurunziza atangaze kuwa angewania urais kwa muhula wa tatu.