China yaorodhesha mabudha halisi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hatua hizo zimechukuliwa ili kukabiliana na mabudha waongo

China imetangaza orodha ya mabudha halisi walio hai ikisema kuwa idadi inayoongezeka ya mabudha wa wahongo wanaotumia jina hilo kupora pesa kutoka kwa waumini.

China imechukua hatua hiyo kwa kuchapisha majina, picha na sehemu waliko mabudha 870 katika mtandao was shirika la habari la Xinhua.

Hatua hiyo imepongezwa na mmoja wa wanaume ambaye ameorodheshwa kwenye orodha hiyo baada kutambuliwa kama Budha aliye hai.

Kulingana na shirika linalohuska na masuala ha kidini nchini China, hatua hizo zimechukuliwa ili kukabiliana na mabudha waongo ambao wanahujumu ubudha eneo la Tibet kwa kuwadanganya waumini na kuwapora pesa.

Hata hivyo hatua hiyo imekosolewa na kutajwa kuwa njama ya kudhibiti masuala ya eneo la Tibet.