Mpiga gitaa na mtunzi nyimbo Glenn Frey afariki

Eagles Haki miliki ya picha Getty
Image caption Frey alisaidia kuanzisha bendi ya Eagles mwaka 1971 akiwa na Don Henley, Bernie Leadon na Randy Meisner.

Mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo Glenn Frey, ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa bendi ya The Eagles amefariki.

Frey, amefariki jijini New York akiwa na umri wa miaka 67 baada ya kuugua wka muda.

Frey alicheza na kuimba baadhi ya nyimbo maarufu zaidi za The Eagles, zikiwemo 'Take It Easy' na'Lyin' Eyes'.

Bendi hiyo iliunganisha mtindo wa pop, rock na country kutengeneza midundo maalum ya California ambayo iliwafanya kuwa maarufu sana miaka ya 1970.

Frey alisaidia kutunga wimbo maarufu wa Hotel California pamoja na mwanabendi mwenzake Don Henley.

Henley, akituma ujumbe wa rambirambi, amemweleza Frey kama mtu mcheshi na mwenye kipaji adimu.

Amesema yeye ndiye aliyechochea wanabendi wengine na kuwasaidia kufanikiwa.