Rais wa Indonesia ataka mabadiliko ya sheria za ugaidi

Joko Widodo Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Indonesia Joko Widodo

Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ametoa wito wa kubadilishwa kwa sheria dhidi ya ugaidi baada ya shambulio la wiki iliopita katika mji mkuu, Jakarta.

Mabadiliko ya sheria hiyo yanayopendekezwa yatazirahisishia mamlaka za usalama wa nchi kumakamata yeyote wanaemshuku kupanga kitendo cha ugaidi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Widodo amependekeza mabadiliko ya sheria ya ugaidi baada ya mashambulizi ya ugaidi mjini Jakarta

Wataruhusiwa kuwashikilia washukiwa kwa muda wa zaidi ya wiki moja bila mashtaka na kuwazuia raia wa Indonesia kujiunga na kupigana na wanamgambo wa Islamc State nchini Syria na Iraq.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashirika ya kiraia yanahofu sheria mpya ya ugaidi itawapa polisi mamlaka zaidi

Baadhi ya vyama vya kisiasa na makundi ya kiraia yanahofu kwamba mabadiliko hayo ya sheria dhidi ya ugaidi yatawarejesha kwenye kipindi cha utawala wa kidikteta Generali Suharto ambapo polisi walikua na mamlaka makubwa.

Watu 12 wametiwa mbaroni kuhusiana na mashambulizi ya risasi na mabomu yaliyosababisha vifo vya raia wawili na washambuliaji watano.