Mwalimu jasiri aaga dunia Kenya

Image caption Sala Farah alikuwa mmoja wa abiria waliokaidi agizo la al shabab

Mwalimu raia wa Kenya ambaye alisifiwa na kuitwa shujaa wakati Waislamu waliwakinga abiria Wakiristo wakati wa shambulizi la al-Shabab kwenye basi moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ameaga dunia wakati akifanyiwa upasuaji kutibu majeraha yake.

Salah Farah ambaye alikuwa naibu mwalimu mkuu katika shule moja ya msingi mjini Mandera, alipigwa risasi wakati yeye na wenzake walipokataa agizo la wanamgambo wa Kiislamu waliowataka abiria kugawanyika kwa makundi mawili ya Waislamu na Wakristo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption al Shabab wamekuwa wakiendesha mashambulizi nchini Kenya

Ujasiri wa abiria Waislamu ambao walikaidi agizo la wanamgambo la kuwataka wajitenge la sivyo wauawe wote ulisambaa kote duniani wakati habari kuhusu shambulizi hilo ziliporipotiwa tarehe 21 mwezi Disemba.

Mwili wa bwana Farah umesafiriswa kwenda mji wa Mandera tayari kwa mazishi.