Baraza la mawaziri latangazwa Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hoteli ya Tobruk lililoko bunge moja la Libya

Baraza la mawaziri limetangazwa la serikali ya umoja wa kitaiafa iliyopendekezwa nchini Libya.

Umoja wa Mataifa umetoa uungwaji mkono mkubwa kwa seriali hiyo mpya kwa lengo la kumaliza miaka kadha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa sasa libya imegawanyika kati ya mabunge mawili hasimu na umoja wa mataifa unataka mabunge hayo yote kuidhinisha serikali ya umoja iliyopendekezwa.

Sasa mabunge hayo yataidhinisha orodha ya mawaziri hao. Lakini bado kuna upinzani kuhusu serikali hiyo katika bunge zote.