Hoteli ya Ritz yashika moto Paris

Image caption Hoteli ya Ritz ndimo alilala Princes Diana usiku wa mwisho kabla afe kwenye ajali ya barabarani

Moto umetokea katika ghorofa ya juu zaidi ya hoteli ya kifahari ya Ritz mjini Paris nchini Ufaransa.

Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa na msemaji wa huduma za moto anasema kuwa jambo muhimu ni kuuzuia moto huo kusambaa

Hoteli ambayo ndimo alilala mwana mfamle wa uingereza Diana usiku wa mwisho kabla akufe kwenye ajali ya barabarani ilikuwa imefungwa kufanyiwa ukarabati na hakuna mgeni alikuwa akiishi humo.

Princes Diana alikuwa akiishi katika hoteli hiyo wakati alikufa mwaka 1997 akiea na mpenzi wake Dodi Al Fayed, ambaye mtoto wa mmiliki wa hoteli hiyo bilionea raia wa misri Mohamed al Fayed.

Ilikuwa ifunguliwe baadaye mwaka huu baada ya kufungwa kwa miaka mitatu ili kufanyiwa ukarabati.