Sakho aharibu gari lake la kifahari

Image caption Diafra Sakho

Mshambuliaji wa klabu ya West Ham raia wa Senegal Diafra Sakho ameliharibu kabisa gari lake la kifahari aina ya Lamborghini lenye thamani ya dola 200,000 kwa kuligongesha kwenye ukuta jijiji London Uingereza.

Image caption Gari aina ya Lamborghini

Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 aligongana ana kwa ana na gari lingine ambapo agari lake lilipoteza mwelekeo na kugonga ukuta karibu na eneo lililo jumba lake la kifahari mashariki mwa London siku ya Jumatatu.

Hi ni kwa mujibu wa gazeti la Standard na Uingereza.