Serikali na waasi Colombia waazimia kufikia amani

ujumbe wa serikali na waasi wa FARC Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wakuu wa serikali i na waasi wa Colombia wa FARC baada ya mazungumzo ya upatanishi yaliyoongozwa na rais wa Cuba Raul Castro(kati kati)

Serikali ya Colombia na waasi wa vugu vugu la mrengo wa kushoto (FARC) kwa pamoja wameuomba Umoja wa Matifa kumaliza mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa nchini mwao.

Wapatanishi wa mzozo baina ya pande mbili katika mazungumzo ya amani nchini Cuba wamesema watauomba Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe wa miezi 12 kusimamia kipindi chochote cha usitishaji mapigano

Umoja wa Mataifa bado haujakubali pendekezo hilo. Pande mbili zimekuwa katika mazungumzo ya amani kwa miaka mitatu.

Wote wamekua wakisema wanamatumaini ya kufikia mkataba wa mwisho wa amani ifikapo mwezi Machi 2016

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapiganaji wa kundi la waasi wa mrengo wa kushoto wa FARC pia wameafiki Umoja wa Mataifa uingilie kati kuleta amani

Mwandishi wa BBC nchini Colombia Natalio Cosoy anasema kuwa juhudi za kuleta amani zinaweza kutekelezwa tu iwapo mkataba wa mwisho utasainiwa

Hata hivyo pande mbili zimesisitiza kuwa tangazo lao hilo ni la maana kulika utaratibu , zikidai linapaswa kutoa ujumbe klwamba mkataba wa mwisho unakaribia, aliongeza mwandishi wetu.

Ni vipi makata utaibadilisha Colombia?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Askari wa serikali ya Colombia akiwa amesimama kando ya kifaru katika mji wa Tame

''Tumeamua kuomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza maafisa wa uangalisi wasio na silaha kwa kipindi cha miezi 12 ," Pande mbili zilieleza kwenye taarifa ya pamoja katika mji mkuu wa Cuba , Havana, Jumanne.

Walisema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa utatoa hakikisho kwamba usitishaji wowote wa mapigano na uwekaji chini silaha utakua wa uhakika, ilieleza ripoti.

Humberto de la Calle, mkuu wa wapatanishi wa upande wa serikali ,alielezea tangazo hilo kama "mafanikio makubwa ".