Dola milioni 5 zatolewa kutafuta chanjo ya Ebola

Utafiti wa Ebola Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Kampuni ya dawa ya Merck itatakiwa kuweka akiba ya chanjo 300,000 za dharura

Muungano wa wa utoaji chanjo, Gavi, umesaini mkataba wa dola milioni 5 kwa ajili ya chanjo ya Ebola , kwa ajili ya kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo hatari siku zijazo.

Mkataba huo unawajibisha kampuni ya dawa ya Merck kutunza chanjo 300,000 tayari kwa matumizi ya dharura ama majaribio ya tiba.

Image caption Watu 11,000 wamekufa kutokana na Virusi vya Ebola katika mlipuko wa hivi karibuni Afrika magharibi

Aidha itawasilisha maombi ya kibali cha chanjo mwishoni mwa mwaka 2017, itakayokuwa hatua itakayofuata katika kuiwezesha kampuni hiyo kuandaa akiba ya dunia ya chanjo.

Zaidi ya watu 11,000wamekufa kutokana na mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola Afrika magharibi.

Kiwango cha mlipuko ambacho ni kikubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ulipelekea kuweko kwa msukumo wa kutafuta chanjo.

Haki miliki ya picha
Image caption Kampuni ya Merck iliongoza majaribio ya awali ya chanjo ya Ebola

Shughuli hiyo ilitarajiwa kuchukua muongo mzima, lakini badala yake ilichukua chini ya kipindi cha mwaka mmoja.

Kampuni ya Merck iliongoza majaribio ya chanjo ya VSV-EBOV - iliyojumuisha chembe chembe za virusi vya Ebola na Virusi vingine salama ili kusaidia mwili kupambana na Ebola.

Ushahidi wa awali kutoka uuchunguzi uliofanyika Magharibi mwa Afrika unathibitisha hayo, ingawa taarifa zaidi bado zinakusanywa.