Pacha wadai rekodi ya Guiness

Haki miliki ya picha Heidi Gannon
Image caption Mapacha sasa - wakiwa na mama yao kutoka kulia Jo, Carol na Heidi

Pacha wawili kutoka Powys, Wales wanatarajiwa kudai rekodi ya dunia ya pacha wa kwanza kuwahi kuzaliwa katika nchi tofauti katika kipindi cha miaka 40 baada ya kutokea tukio jingine la aina hiyo.

Heidi Gannon alizaliwa katika hospitali ya Welshpool mnamo mwaka 1976, huku dada yake kwa jina Jo Baines akizaliwa eneo la Shrewsbury, England karibu saa mmbili baadaye.

Guinness World Records ilikuwa imewaorodhesha watoto wengine pacha waliozaliwa Scotland na England mnamo mwaka 2012 kama wa kwanza kabisa hadi walipowasiliana na Bi Gannon.

Baada ya kufanya uchunguzi wake, Guinness ilisema kuwa pacha hao kutoka Wales kweli walivunja rekodi hiyo.

Bi Gannon alibaini madai ya vijana wake ya kuvunja rekodi hiyo baada ya kununua kitabu kwa ajili ya kijana wake.

Haki miliki ya picha Heidi Gannon
Image caption Mapacha walipozaliwa mwaka 1976

Alizaliwa 09:00 GMT (saa sita asubuhi Afrika Mashariki) tarehe 23 Septemba mwaka 1976 katika hospitali ya Welshpool eneo la Powys, lakini mama yake Carol Munroe hakufahamu kuwa alikuwa na ujauzito wa watoto wawili.

Dada yake Bi Baines, alizaliwa baadae saa 10:45 GMT (Saa nane kasorobo Afrika mashariki) kilomita 32 ndani ya England, katika jimbo la Shropshire.

Maafisa walithibitisha kuwa walikua wanasubiri rekodi itayarishwe na kwamba walikua wakiwasiliana na Bi Gannon kuhusu hilo.

Msemaji wa Guiness alisema: "tulifahamishwa kuhusu dai la Bi Baines na Bi Gannon la rekodi hii wiki iliopita na baada ya utafiti fulani uliomuhusisha mshauri wetu wa masuala ya mapacha tumeweza

kuthibitisha kwamba kweli hawa ni mapacha wa kwanza kuzaliwa katika nchi tofauti."