Caitlyn Jenner kuzindua kitabu cha maisha yake

Caitlyn Jenner Haki miliki ya picha AP
Image caption Caitlyn Jenner atazindua kitabu cha kumbu kumbu ya mabadiliko ya maisha yake

Caitlyn Jenner anatarajia kuzindua kitabu cha kumbu kumbu ya kipindi cha mabadiliko ya maisha yake.

Kitabu hicho kitaandikwa na mwandishi wa habari na vitabu - Buzz Bissinger, ambaye alisema aliombwa kufanya mradi huo miezi michache baada ya makala ya jarida la Vanity Fair kufichua maisha ya Caitlyn Jenner kwa dunia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kitabu cha Jenner hakitasaza lolote kuhusu maisha yake

Alisema alimwambia Jenner kwamba "hakuna chochote kitakachoachwa'' " na kwamba anampango wa kuwahoji "makumi ya watu ".

"ni kitabu chake, lakini kitaripotiwa kote kwa ajili ya kuhifadhi ukweli wake. Amekuwa muwazi vya kutosha , na nadhani litakuwa suala muhimu litakalokifanya kitabu chake kuwa muhimu ."

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kitabu cha Caitlyn Jenner kitaangazia pia ndoa, na uhusiano na wanae

Kitabu hicho - kinachotarajiwa kutolewa mnamo mwaka 2017 - kitaangazia maisha yake kama Bruce Jenner, yakiwemo maisha yake kama mwanariadha ,ndoa na mahusiano yake na wanae, na pia kipindi cha mabadiliko yake ya maumbile kuelekea Caitlyn wa sasa.

Jenner alisema : ''Mambo yamekua yakienda mbio, kiasi kwamba itakua vema sasa kupunguza kasi ya mambo kidogo na kuchukua muda unaofaa kutathmini safari ya maisha yangu''