Lupita Nyong'o azikosoa tuzo za Oscars

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lupita ameikosa Oscars kwa kutowateua wacheza filamu weusi

Mcheza filamu raia wa kenya Lupita Nyong'o ameungana na wacheza filamu wengine kushutumu kutojumuishwa kwa wacheza filamu weusi au wale wachache kutoka kwa orodha ya wale wanaowania tuzo za Oscars.

Katika akaunti yake ya Istagram Lupita amesema amekasirishwa sana na kukosa kujumuishwa kwa wacheza filamu weusi.

Image caption Jada pinket Smith(kulia) anasema hatahudhuria tuzo za Oscars

Mwaka 2014 Lupita Nyong'o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu ya Twelve Years a Slave.

Anaungana na wacheza filamu wanaozidi kuongezeka wakiwemo David Oyelowo na Don Cheadle ambao wamekosoa tuzo za Oscars kuwa kukosa kuteua watu kutoka tabaka zote.