Mos Def aapa kutorejea Afrika Kusini

Image caption Mos Def amezuiwa kuondoka Afrika Kusini kutokana na tatizo la cheti chake cha kusafiria

Mwanamuziki raia wa Marekani Mos Def ambaye pia anafahamika kama Yasiin Bey ameapa kuwa kamwe hatarejea nchini Afrika Kusini wakati ataruhusiwa kuondoka nchini humo.

Kwa sasa Bei yuko mjini Cape Town baada ya utawala kumzuia kuondoka kutokana na tatizo lan cheti chake cha kusafiria.

Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vinasema kuwa mwanamuziki huyo ametoa wito kwa wanamuziki wenzake kutoizuru Afrika Kusini.

Anaanza kutoa ujumbe wake akiimba na kusema kuwa, "Tafadhalia waambie hakuna mchezo Afrika Kusini ambapo anaendelea na kuahidi kuwa kamwe hawezi kurudi Afrika Kusini.

Anaendelea kusema" kwa sasa niko Afrika Kusini na ninazuiwa kuondoka bila sababu yoyote.

Hata hivyo serikali ya Afrika kusini imejitetea na kusema inafuata sheria za uhamiaji.