Abba wajumuika pamoja Stockholm

Abba
Image caption Wanamuziki hao walitumbuiza pamoja mara ya mwisho 1986

Wanachama wote wanne wa kundi la muziki la Abba walijumuika tena pamoja kwa sherehe ya ufunguzi wa biashara mpya mjini Stockholm.

Ukumbi huo wa burudani, ambao umejengwa kwa kufuata mfano wa hoteli ya Kigiriki katika filamu ya Mamma Mia!, umetokana na wazo la nyota wa Abba Bjorn Ulvaeus.

Aliungana na wenzake Benny Andersson, Anni-Frid Lyngstad, na Agnetha Faltskog sherehe ya kufunguliwa kwa ukumbi huo.

Wanne hao walionekana pamoja mara ya mwisho wakati wa kuzinduliwa kwa filamu ya Mamma Mia! London na Stockholm mwaka 2008.

Mashabiki na wageni walilipia tiketi £110 ($157) kuhudhuria sherehe ya kufunguliwa kwa ukumbi huo.

Abba hawajawahi kutumbuiza umma pamoja tangu1986.

Walivuma kwa nyimbo kama vile Take a Chance on Me, Fernando, Waterloo, Knowing Me Knowing You na Mamma Mia.