Ujumbe wa UN kumaliza ghasia Burundi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ghasia nchini Burundi

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unawasili nchini Burundi ili kujaribu kumaliza ghasia zinazoendelea kushuhudiwa nchini humo na kuunga mkono mazungumzo ya amani.

Uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania urais mwezi Aprili ulisababisha maandamano na mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.

Haki miliki ya picha un.org
Image caption Mkutano wa baraza la umoja wa mataifa kuhusu usalama

Mwandishi wa BBC anasema kwa ujumbe huo unatarajiwa kuishawishi serikali ya Burundi kukubali kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika ili kuzuia vita vya kikabila na ukiukaji wa haki kibinadamu.