Elimu:Mfumo wa GPA wafutwa Tanzania

Image caption Elimu Tanzania

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amefuta rasmi mfumo wa kukokotoa matokeo kwa mtindo wa GPA.

Ameagiza matokeo ya kidato cha 4 na 6 yatolewe kwa mfumo wa madaraja (divisions) kama ilivyokuwa hapo zamani.Maamuzi haya yanakuja baada ya waziri huyo kuwapatia baraza la mitihani, wiki moja kuumpa sababu za kubadili mfumo wa utunuku viwango vya ufaulu wa awali na kwenda kwa wastani wa pointi (GPA) unaotumika sasa Kidato cha Nne na Sita.

Waziri Ndalichaki amesema amefikia uamuzi huo baada ya Baraza la Mitihani (NECTA) kushindwa kutoa utetezi wa kisayansi juu ya sababu zilizopelekea wao kubadili mfumo wa upangaji madaraja ya ufaulu kwa wanafunzi

Mfumo wa GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka 2014 ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana. Mwaka 2013, ya asilimia 60 ya wanafunzi wa kidato cha nne walifeli mitihani wa kitaifa, hali ilioleta kwa matokeo hayo kurudiwa tena ili kuwafaulisha wanafunzi zaidi.