Magufuli amteua Kikwete mkuu wa chuo

Kikwete
Image caption Dkt Kikwete alistaafu baada ya kuongoza Tanzania kwa mihula miwili

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amemteua Rais mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Tangazo la uteuzi huo limetolewa na katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Uteuzi huo umeanza kutekelezwa tarehe 17 Januari.

Balozi Nicholas Kuhanga amekuwa akishikilia wadhifa huo kama kaimu, kwa mujibu wa tovuti ya chuo kikuu hicho.