Ongwen 'aliwagawa wanawake na wasichana'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ongwen

Waendesha mashtaka bado wanaendelea kutoa ushahidi wao kwamba aliyekuwa kamanda wa LRA Dominc Ongwen alihusika na uhalifu wa kivita.

Mashahidi wanasema kuwa kamanda huyo aliwagawanya wanawake na wasichana kwa wanaume waliokuwa katika jeshi lake kulingana na viongozi hao wa mashtaka.

Shahidi mwengine amesema kuwa Ongwen alikuwa na uwezo wa kutekeleza hilo bila ya idhini ya kiongozi wa LRA Joseph Kony ambaye angemwelezea.

Image caption Raia wakifuatilia kesi hiyo kutoka nchini Uganda

Awali,ushahidi ulitolewa ili kuonyesha jinsi jeshi la Uganda lilivyoingilia mazungumzo kati ya makamanda hao wa LRA.

Mwandishi mmoja katika mahakama hiyo alituma ujumbe wa Tweeter uliosoma ''Kony alimpongeza sana Dominc kwa kazi yake nzuri''.