Filamu mpya ya Star Wars kuchelewa

Filamu Haki miliki ya picha AP
Image caption Filamu hiyo mpya ilikuwa imepangiwa kutolewa Mei 2017

Kampuni ya Disney imetangaza kwamba filamu mpya ya Star Wars ambayo ilipangiwa kutolewa baada ya The Force Awakens itachelewa.

Filamu hiyo nambari nane katika mwendelezo wa filamu za Star Wars ilipangiwa kuzinduliwa mwezi Mei 2017 lakini sasa itazinduliwa mwishoni mwa mwaka huo, sana mwezi Desemba.

Filamu ya The Force Awakens, ambayo ni ya saba, ilizinduliwa mwezi uliopita na imeendelea kuvuma duniani.

Wiki tano baada ya kuanza kuonyeshwa katika kumbi za sinema, imezoa $861m (£607m) nchini Marekani na $1.88bn duniani.

Haki miliki ya picha Getty

Disney hawajasema ni kwa nini filamu hiyo itachelewa lakini kuna habari kwamba huenda hadithi yenyewe inafanyiwa marekebisho.

Fimalu hiyo itaanza kuandaliwa mwezi ujao katika Pinewood Studios, magharibi mwa London.

Tarehe hiyo mpya ya kutolewa kwa filamu hiyo ina maana kwamba huenda ikapatana sokoni na filamu nyingine inayosubiriwa kwa hamu na ghamu, Avatar 2, ambayo imepangiwa kutolewa Krismasi 2017.