Maandamano yaendelea Tunisia

Haki miliki ya picha getty images
Image caption Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi

Maandamano ya vijana walioghadhabishwa na hali ya ukosefu wa ajira yamesambaa katika miji mbalimbali nchini Tunisia,hali iliyosababisha kifo cha askari mmoja wakati wa makabiliano siku ya Alhamisi.

Maandamano yalianzia kaskazini mwa mji wa Kasserine baada ya mtu mmoja kujiua baada ya kukosa ajira serikalini

Hali ya ukosefu wa ajira imekuwa mbaya zadi tangu baada ya mapinduzi ya mwaka 2011, Rais Zine al-Abidine Ben Ali alioondolewa madarakani.

Baadhi ya waandamanaji wamesema kuwa matatizo mengi ya kijamii hayajashughulikiwa tangu mwaka 2011.

Rais Beji Caid Essebsi alisema kuwa zaidi ya nafasi za kazi 6,000 zitatolewa kwa watu wa Kasserine.Serikali pia imeahidi kufanyia uchunguzi shutuma za rushwa.