Brazil:Watoto zaidi waathiriwa na kirusi cha Zika

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watoto waathiriwa na ugonjwa wa zika nchini Brazil

Mfumo wa afya nchini Brazil unakabiliana na mlipuko wa ugonjwa unaothiri ubongo wa watoto nchini Brazil.

Mamlaka inaamini ugonjwa huo unasababishwa na kirusi cha zika kinachosambazwa na mbu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mbu anayesambaza virusi vya Zika

Kumekuwa na takriban visa 4000 vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa huo tangu mwezi Oktoba,wakati mlipuko huo ulipoanza na visa vingine 500 katika kipindi cha juma moja pekee.

Kirusi hicho cha zika kimeenea nchini Brazil na sasa kimeanza kupatikana katika mataifa ya kusini mwa Marekani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kifaa kinachopima viini vya zika

Serikali ya Brazil imetenga fedha za ziada kusaidia utengezaji wa chanjo pamoja na kipimo kipya.