Ethiopia yashinda medali zote Dubai

Image caption Tirfi Beyene(kushoto) na Tesfaye Dibaba

Wanariadha wa Ethiopia wameshida dhahabu zote mapema leo katika mashindano ya marathon mjini Dubai ambazo ndizo mbio zenye malipo bora zaidi duniani.

Tesfaye Abera Dibaba alimaliza wa kwanza katika mbio za wanaume kwa muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 24 ambao ni muda wake bora.

Katika mbio za wanawake Tirfi Tsegaye Beyene alimaliza wa kwaza kwa muda wa saa mbili dakika 19 na sekunde 41 ambayo ni mara ya pili ameshinda mbio hizo na kutunukiwa kitita cha dola 200,000.

Hi ndiyo orodha ya ushindi ya wanariadha wa Ethiopia.

Wanaume:

Tesfaye Abera Dibaba 2:04:24 Lemi Berhanu Hayle 2:04:33 Tsegaye Mekonnen Asefa 2:04:46 Sisay Lemma Kasaye 2:05:16 Mula Wasihun Lakew 2:05:44.

Wanawake:

Tirfi Tsegaye Beyene 2:19:41 Amane Beriso Shankule 2:20:48 Meselech Malkamu Haileyesus 2:22:29 Sutume Asefa Kebede 2:24:00 Mulu Seboka Seyfu 2:24:24.