Valls ataka Ulaya idhibiti mipaka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Amesema kuwa ulaya inastahili kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti mipaka yake ya nje

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amaeonya kuwa tatizo la uhamiaji lililo barani ulaya linahatarisha muungano wote wa ulaya.

Bwana Valls ameiambia bbc kuwa ulaya haiwezi kuwachukua wakimbizi wote wanaokimbia vita vibaya nchini Iraq na Syria.

Zaidi ya wahamiaji milioni moja, wengi wakimbizi waliwasilia barani ulaya mwaka uliopita wakifanya sarafi hatari. Ijumaa takriban watu 21 waliuawa wakati mashua zao zilizama nje ya visiwa vya Ugiriki.

Image caption Zaidi ya wahamiaji milioni moja waliwasili ulaya mwaka uliopita

Bwana Valls pia alisema kuwa ufaransa itathmini kudumisha hali ya hatari iliyotangazwa hadi pale vita dhidi ya kundi la Islamic State vitakapokwisha.

Hatua hizo zilitangazwa baada ya Islamic State kuendesha mashambulizi mji Paris tarehe 13 mwezi Novemba na kisha kuendelea kwa miezi mitatu zaidi.

Amesema kuwa Ulaya inastahili kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti mipaka yake ya nje.