Gates aipongeza Ethiopia

Haki miliki ya picha NAWAL
Image caption Bill Gates na mkewe Melinda Gates

Mtu tajiri zaidi duniani Bill Gates ameipongeza Ethiopia kwa kuwachukua wakimbizi.

Bilionea huyo ameiambia BBC kuwa anafikiri kuwa maendeleo ya kiuchumi yatazuia wimbi la wahamiaji kutoka nchi zingine.

Alipongeza Ethiopia ambayo ilikuwa chanzo cha wakimbizi lakini sasa ndiyo imewachkua wakimbizi wengei kuliko nchi yoyote ile.

Gates anasema kuwa hii ni kutokana na sababu kuwa kumekuwu na uwekezaji katika kilimo, serikali zina sera nzuri na kuna uzalishaji mkubwa wa chakula.

Gates ambaye alikuwa akizunguzma mjini Davos ana wakfu mkubwa zaidi duniani.