Waghana walalama mitandaoni kuhusu bei

Image caption Ghana walalama kuhusu kupande kwa bei za vyakula

Raia wa Ghana waliopo katika mitandao ya kijamii wanapinga kuongezeka kwa kodi pamoja na bili za huduma mbali mbali kwa kuvaa nguo nyekundu.

Watu wamekuwa wakionyeshana nguo wanazofaa katika mtandao wa facebook.

Jonathan Asare ameelezea katiua mtandao wake wa facebook kwa nini alikuwa anavalia nguo nyekundu siku ya ijumaa,akitaja neno la Ghana la 'dumsor' linalomaanisha ''kuwasha na kuzima'' kufuatia kukatika kwa umeme.

Vijana wa taifa hili wana tamaa lakini ukosefu wa kazi unatuathiri moja kwa moja.Hii ni Kwa sababu:

1.Dumsor ameharibu viwanda vyetu na kampuni

2.Viwango vya riba vya juu vya asilimia 30

3.Sarufi ya Ghana

4.Viwango vya kodi vya juu

5.Ushuru wa viwango vya juu.

Image caption MItandao ya kijamii

Pingamizi hiyo inaongozwa na kundi moja la wanaharakati Occuppy Ghana ambalo limeongeza athari zaidi katika orodha hiyo.