Amazon kuwarejeshea fedha wanunuzi wa 'hoverboards'

Haki miliki ya picha Novus Ordo
Image caption Kiongozi wa dini aliyevaa hoverboard kanisani

Bodi moja ya serikali ya Marekani imesema kwamba duka la Amazon linalotekeleza shughuli zake kupitia mauzo ya mitandaoni limejitolea kuwalipa wateja wake walionunua vibao vyenye magurudumu vinavyotumiwa sana na vijana kutembelea,kulingana na tume ya usalama wa bidhaa.

Hitilafu za kimitambo katika vibao hivyo ndio iliyosababisha kuchomeka kwa maeneo mbalimbali nchini humo.

Tume hiyo kwa sasa inawachunguza watengenezaji 13 wa vibao hivyo kuhusu usalama wake.

Awali Amazon ilikuwa imesitisha uuzaji wa vifaa hivyo kufuatia maswali mengi juu ya usalama wake.

Haki miliki ya picha Changzhou First International Trade
Image caption Hoverboard

Mbali na jina hoverboard,vibao hivyo haviruki bali vina magurudumu ambayo umuhitaji mtu kusimama vinapokwenda.

''Ninataraji wafanyibiashara na watengenezaji wa vibao hivyo watachukua hatua na kurejesha fedha kwa wateja wao,alisema mwenyekiti wa tume hiyo Elliot F Kaye katika taarifa.

Ninatarajia kwamba wafanyibiashara wengi wa mitandaoni pia kusitisha kuuza bidhaa hizo hadi pale tutakapokuwa na uhakika kuhusu usalama wake.